PERAMIHO NA VIVUTIO VYAKE VYOTE , TAZAMA KANISA KUBWA LILILOKO PERAMIHO SONGEA.KANISA KONGWE TZ
PeramihoPeramiho is located in TanzaniaPeramihoPeramiho
Mahali pa Peramiho katika Tanzania
Majiranukta: 10°38′8″S 35°27′44″E
Nchi
Tanzania
Mkoa
Ruvuma
Wilaya
Songea Vijijini
Idadi ya wakazi
- Wakazi kwa ujumla
15,031
Peramiho
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,031 waishio humo. [1].
Abasia na parokia
Edit
Inajulikana hasa kutokana na abasia ya wamonaki Wakatoliki Wabenedikto.
Abasia hiyo ilianzishwa kama kituo cha umisionari na P. Cassian Spiess O.S.B. aliyefika Peramiho mwaka 1898.
Mnamo mwaka 1931 Peramiho ilifanywa kuwa abasia na pia makao ya jimbo chini ya Abate-Askofu Gallus Steiger O.S.B..
Makao ya jimbo yalihamishiwa Songea mnamo mwaka 1969, na siku hizi kuna majimbo matatu (Jimbo kuu la Songea, Jimbo Katoliki la Njombe na Jimbo Katoliki la Mbinga) yaliyotokana na jimbo la zamani la Peramiho.
Peramiho kuna shule na hospitali nzuri pamoja na monasteri.
Pia ni makao makuu ya parokia ya Peramiho ambayo ina vigango vifuatavyo: Parangu, Lilambo, Likuyu, Mwanamonga, Litowa, Nakahuga, Sinai, Maposeni, Mdunduwalo na Morogoro.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
#daressalaam #shorts #funny #peramiho